MAARIFA INAPIGANA NA UOGA

KATIKA MWAKA UNAOKUJA.”

Maneno yametoka kwa Alan Watt.

Desemba 25, 2007

cuttingthroughthematrix.com

alanwattsentientsentinel.euHamjambo. Mimi ni Alan Watt na hii Cutting Through the Matrix katika Desemba 25, 2007. Nyinyi ambao mnaweza kumbuka, utaona ati na kila krismasi vitu zinaendelea kuwa za kioja, kioja kwa ati tunapitia mambo yale ya mara kwa mara, mingi ambayo ni mpya kwa jamii, ununuaji na kupatiana zawadi, kadi na kutoa mvuke. Kwa kweli hiyo ndiyo sehemu kubwa yake kwasababu ni kutoa mvuke kutoka kwa mwaka iliyojaa na shida za kawaida za binaadamu na kuongezea kwa hiyo tuko na shida za huu mfumo ambazo zimekuwa zetu.


Wanahakikisha kwa hiyo kabisa tunapoharakisha kwa hii dunia moja iliyo na njia yya kuishi ya kiimla na kuangalia na kuona na kuchunguza. Hii ni habari mbaya. Habari mbaya kwa sisi sote. Na zaidi hivyo bila shaka kwa wale ambao wanajua. Kwa wale ambale hawajui wanasema ati ujinga ni neema. Neema yao ni kukosa kujua ajenda yote. Hawaishi kwa kweli hawa watu. Wanaelea kwa maisha kama wanyama wa silika, lakini wale ambao wanajua na ambao hisia, hisia zao za kujikinga bado zinafanya na ambao wamegundua kinachoendelea na wanaoweza kuona mabadiliko yanayoendelea kando yao, tunajua kitu siyo mzuri inakuja.


Na katila muda huu wa miaka napata watu ambao wamekuwa wakifuata ajenda ya dunia na shida ya kubwa ni kutengwa. Kwa hiyo namaanisha watu kama hao ambao wametengwa na wametawanyika katika dunia. Itakuja kwa steji ambayo wale ambao wanajua kinachoendelea itabidi wawasiliane na wenyewe tunapopitia hii yote ili tubaki na akili timamu, kwasababu si rahisi kujua lakini inabidi uishi kwa mali ya waliokufa. Waliokufa kuwa wale kando yako wanaopitia njia zile ya mara kwa mara kama wanyama wa silika na hawaulizi mingi kuhusu chochote. Haibidi. Haibidi wafikirie chochote kwa njia yoyote.. Wamelelewa na sisi soe pia kwa jamii ambayo mabingwa wanatufanyia fikra yetu yote, na tumefunzwa kuiamini na sasa tuko na wengi kwa umma wanaiamini. Wanaamini ati si lazima wafikirie sana. Wanaamini ati kazi yao ni kuzalisha, na kuona televisheni na kufurahia kama watoto wa kila saa.


Niliona mabadiliko zilizoelekea katika uunganisho wa Ulaya. Niliishi kwa wingi wake na kwa masafiri zangu katika nchi hizo niliona ati sheria zilikuwa zinapita katika kila nchi na serikali zao, bila kusema ati kila nchi ingine ilikuwa inazipitisha kwa muda sawa na yote ni kufanya na kufananisha mifumo zao wakitayarisha kuziunganisha. Wanasiasa waliambiwa wadaganye umma na wamekuwa wakifanya hivyo tangu 1948 walipotengeneza tume za urasimu katika kila nchi zilizokuwa zifanye kwa siri kuelekea jumuiya. Hivyo ndivyo vitu zinafanyika kwa dunia ya ukweli.


Kwa wale ambao wanaamini kwa njia fulani tumekuwa na hii binguni zamani na watumishi wa umma, hiyo ni hadithi mzuri kuamini lakini ni kinyume ya ukweli. Mipango kubwa za serikali na za nchi huwa zinawekwa kutoka kwa umma kila saa, ata kama unaweza ona athari zake zikifanyika maishani. Unaweza athari zake kila mahali kando yako. Wadanganya hadi mwishowe. Hivyo ndivyo wanafanya na hiyo ndiyo ukweli kuhusu maserikali. Hatujawai kuwa na tunachoangalia kama demokrasia. Haikuwa popote. Sanaa ya kutawala ni kuambia yote ambayo wanahitaji kujua ili washirikiane na ajenda, ambayo huwa inatawalwa na wananguvu wachache.


Nilishangaa vile watavyoingiza Marekani kwake. Nilijua wangekua moja wa injini kuu zinazofanya kuilekea kwasababu ya nguvu ya watu, watu wengi marekani na rasilimali zake kando yake, watu wa kulipa kodi kuileta, na mfumo wa elimu ya vyuo vikuu ambapo unaweza chagua yule unayotaka kuleta juu kwa ngazi kwa hizi uajenti zinazofanya kuelekea serikali ya dunia. McCarthy hakukosea kusema vitu kubwa zilikuwa zinafanyika. Aliona waliothani ni wakomunisti wakisonga kwa wingi kwa idara ya nchi, lakini hakujua picha yote ati hii ilikubaliwa. Ilikuwa mpango wa kitambo. Lazima kwanza uweke nguvu pahali moja na hapo ndipo nadharia za Marx zilitumiwa na Magharibi na hivyo kwasababu hao ndio walifadhili Marx. Fikra ilikuwa kwanza ungekuwa na vita za uhuru, uhuru wa taifa. Hiyo ndiyo ilikuwa lengo walichosukuma, kwa hivyo ulisukuma kwanza utaifa alafu ukishaifikia ungejaribu kupatia serikali nguvu yote. Nguvu kwa mamlaka wa kati kati. Tulipata hiyo na vita ya wenyewe Marekani ambapo Lincoln alitangaza sheria ya kijeshi alafu akachukua nguvu yote.


Tuliona hiyi ikifanyika katika nchi za Vita za Dunia ya Kwanza na ya Pili. Hizo nchi saha Uingereza zilichukua nguvu yote ya ujenzi, ukulima, kwa kila kitu kinachoongoza maisha yako ilienda kwa mikono za serikali na chini ya mamlaka yao. Walipofaulu hapo walifanya kuelekea uunganisho na nchi zingine, kama biashara wakati ambapo zinajinyakua kwa wenyewe, vita ya kibiashara. Fikra sawa. Wengi wa umma, ata kama wangeweza kuiona kidogo, hawawezi kuelewa mingi. Wanaweza kuelewa vile asili ya binaadamu iko hadi hapo na huwa kuna hawa watu ambao wako na njaa ya nguvu, ambao watapanga vitu kwa njia yao, waifanye na waishi kama wafalme juu yako. Wanaweza elewa hiyo sehemu yake, lakini hawaelewi sayansi za propaganda kubwa ambayo sote tumekuwa nayo ili tusione iliyo mbele yetu kwa wale ambao wameamka.


Majeruhi wako kila mahali kando yako na watu wengi ni majeruhi wa haya mafunzo, ambapo ata muda wako wa huru ambapo unathani unaburudishwa kwa kweli inaingiza kwa akili maajenda na fikra ambazo haungekujia kwa mwenyewe, hitimisho zilizoandikwa kwa makini katika hizo hadithi na mipango za sinema zenu na kuendelea na mabingwa. Zinabadilisha maoni yako ya kila kitu lakini hatimaye kubadilisha maoni yako kuhusu kilichokuwa utakatifu wa maisha. Unapomeza propanganda na tumekuwa na wingi wake kuanza na programu za asili alafu pahali ya wanyama kwa ufalme wa dunia. Alafu pole pole wanatuingiza kwa hiyo picha hadi tumekuwa tu mnyama mwengine alafu ukianza tu kuamini hiyo umeshindwa. Umeshindwa na watu wameshaikubali, ati wewe ni mnyama mwengine na kwa hivyo hautajali sana wakikuja kuwamaliza.


Hapa kuna mfano mzuri ya hizi mbinu zikionyeshwa kwa wazi na mtu ambaye bila shaka anaweza kuziona. Inatoka kwa L.A Times, Desesmba 10, 2007. iliandikwa na Gregory Rodriguez na inaitwa “ Greening of the Zeitgeist” katika ukurasa wa 15. Inasema:

“Ndoa yako iko na shida? Unapigana kila saa na mpenzi wako? Hamu imeisha? Utafiti mpya iliyochapishwa na Chuo ya Masayansi za Kitaifa inasema ati pengine unafaa kufikiria mara ya pili kabla utaliki. Hapana, si kwasababu ya athari mbaya ambayo inayoweza leta kwa watoto ama ata mfuko wako, lakini itachofanyia mama wako. Mama Dunia. Mchezo kando matokeo ya utafiti huu ina mantiki. Kwasababu wanagawana rasilimali, watu kwa nyumba za ndoa wanatumia nguvu na maji kwa ufanisi zaidi kushinda waliotaliki. Lakini hiyo utafiti inaonyesha pia kwa kiasi gani geuko la hali ya hewa duniani pamoja na ugaidi


Alan: Hii hapa ni muhimu.

“... imechukua pahali pa Umoja wa Kisovyeti kama hayawani iliyo chini ya kitanda katika fahamu la taifa yetu. Imefika kiwango cha (kuwa fikira inayofafanua muda huu wa historia), ikiwa na athari ya kichini kwa maadili na dini.”


Alan: Anakuambia ukweli hapo, ukweli muhimu sana kwasababu lazima wawe na vita isiyoisha ama kitu. Nimesoma kutoka “The First Global Revolution”(Upinduzi wa kwanza wa Kidunia) iliyoandikwa na Club of Rome(Klabu ya Rome) na waanzishaji wake waliandika hii kitabu, iliyochapisha katika mwanzo wa miaka za 1990. Wanakuambia kwake ati ilikuwa katika miaka za 1970 ndiye hii kikundi ilikubali hao ndiyo walianzisha fikra ya Ongezeko la Joto Duniani kuwa kama adui na hatimaye binaadamu mwenyewe ndiyo alikua adui kwa kuisababisha na hivyo ndivyo wangeleta dunia pamoja na waingoze kwa hii ajenda mpya – Ajenda ya Dunia Mpya.


Kurudi kwa hii gazeti kutoka L.A Times, Nitarudia hiyo sehemu ya mwisho.


“Utafiti huu inaonyesha pia...”


Alan: Hii inatoka kwa Chuo cha Masayansi za Kitaifa.


“... inaonyesha kwa kiasi gani geuko la hali ya hewa duniani pamoja na ugaidi imechukua pahali pa Umoja wa Kisovyeti kama hayawani iliyo chini ya kitanda katika fahamu la taifa yetu. Imefika kiwango cha (kuwa fikira inayofafanua muda huu wa historia), ikiwa na athari ya kichini kwa maadili na dini.”


Alan: Iko na udini. Ulithani ati Mwendo wa Kijani ilikuwa tu wanahifadhi na ajenti za fikira zinazowafadhili – ni dini unaona. Lazima watengeneze dini.


“Tishio za taifa za kale – ata uoga wa bomu la atomu – wingi wake ilikuwa katika siasa. Wengi pengine walikuwa na wasiwasi kuhusu vita ya nyuklia, lakini ilingia kwa maisha yao ya kibinafsi kila mara kwa wakati. Si wengi wetu walitengeneza kimbilio za bomu kwa nje ya nyumba zetu. Lakini nuoga wa geuko la hali ya hewa iko kwa maisha zetu za kila siku za kibinafsi. Kwasababu ongezeko la joto duniani na juhudi za kuisimamisha zinashika karibu kila sehemu ya sera, mazingira imekuwa kichungi cha maadili ambapo kila kitu kingine kinachujwa. Kama au si wanajali juu ya mazingira, wanakundi wa kila aina wanaitumia kujimanufaa kimaadili. Sasa ata wale wasiokubali na talaka wako na usaidizi wa mazingira...”

“Kuna mifano mingi zaidi. Kwa Julai, ripoti ya mazingira iliyotolewa na idara ya uongozi wa mali kutoka magharibini ilikubaliwa haraka na wanaharakati wanaokataa uhamiaji kwasababu ilipata ati wahamiaji wasiokuwa na hati walikuwa tishio ya kiikolojia kwa mali za umma huko Arizona Kusini – walipovuka jangwa kwa wingi, waliharibu ikolojia hiyo. Wanaopinga walijadili ati ongezeko wa kijeshi kwa mpaka ilikuwa tishio kubwa zaidi kushinda wahamiaji wenyewe. Geuko la hali ya hewa imeingia ata sehemu ya siasa ya ngono. Mwezi uliopita mwanasayansi mwanamke kutoka Sweden...”


Alan: Sikiza hii hapa, na nimekuwa nikisema kwa miaka na nimesoma kutoka kitabu ya Gorbachev pia, alipoongea kuhusu kufanya huu mwendo wa kijani iwe dini na vile kila kitu zingekuja kusaidia Mama Dunia. Nimekuwa nikisema kwa miaka ati watu wamefundishwa kutoka miaka za kwanza ati watatoa uwezo wa kuzaa kwa hiari, ambacho ni kile wakuu wanataka pia, kumbuka, kupunguza idadi ya watu.


“Geuko la hali ya hewa imeingia ata kwa sehemu ya siasa ya ngono. Mwezi uliopita, mwasayansi mwanamke kutoka Sweden alipata ati” wanawake wanatoa gesi ya kaboni kwa udogo kushinda wanaume...”


Alan: Tena, kudhibiti idadi ya watu.


“... Ilitoa karatasi iliyoonyesha ati kama wanandoa wangezaa watoto wawili badala ya watatu,”wangeweza kukata utoaji wao wa gesi za kaboni kiasi inayotoshani na ndege 620 za kurudi kutoka London hadi New York kwa mwaka moja.”


Alan: Hiyo ni mingi sana, nitasema.


“Hivyo, mwezi uliopita gazeti ya London ilionyeshi mwanamazingira wa miaka 35 aliyeuliza kutolewa uwezo wake wa kuzaa ili asaidie kwa juhudi ya “kuokoa sayari.”


Alan: Hapo ndipo wewe. Inaanza kuchosha kwangu unapojua kinachokuja. Ni kama kuona sinema mara ya pili. Huyu ndiyo huyo mwanamke. Hii ndiyo anasema.


“...Kuwa na watoto ni kujifikira binafsi,” alisema. “Inahusu tu kukinga jenii yako katika gharama ya sayari.


Alan: Hiyo ni kabisa walichokuwa wakisema watafanya watu waamini, nyuma katika miaka za kwanza za 1900.


“Nyingi za tishi za nje zinatukumbusha juu ya uzuri wetu, Ajenti zilizonyuma yao ni adui wetu, watu wabaya. Njia ya kuzungmza ya wanamazingira kwa mikono nyingine inatukumbusha kila saa juu ya wajibu wetu.


Alan: Kumbuka Klabu ya Rome, tutalawama umma na tuwafanye waiaminii.


“Kwa hiyo sababa, umazingira iko karibu zaidi kwa kuamka wa kidini kushinda fikra ya kisiasa. Kama wainjili, wanamazingira wanaongea kwa njia yao juu ya moto. Kama mhubiri, mwanaharakati wa mazingira, anadai tujipatie kwa kitu iliyo zaidi yetu na tufanye toba kwa badhiri na dhambi za kaboni zetu. Kama kanisa ya kikatoliki ya kitambo, wanauza ata anasa – kabiliano za kaboni.”


Alan: Ndipo hapo kodi zenu za kabiliano za kaboni.


“Na kama dini yoyote inayotia mkazo kwa dhambi, waja wake watatafuta njia zote za kudokeza haki yao ya kibinafsi. Saha katika msimu wa krismasi wa kununua, ni ya furaha kuona hii dini mpya ya kidunia ikigongana na zile ambazo zimekuwa hapa: ununuaji. Wiki uliopita tu, nilipata ilani wa upya kutoka gazeti la habari ninayopenda, ili ahadi ati kama ningefufua chango changu sasa( na kwa hivyo ningezuia wanaozichapisha kunitumia makaratsi 10 zaidi za makumbusho), ninge fanya upya dunia pia kwa muda sawa. Na hiyo tu ni bakshishi ya barafu.


Wauzaji na watengenezaji wengi wanaonyesha bidhaa zao kama zisizo haribu mazingira, si kwasababu zitasaidia dunia lakini kwasababu itakufanya uhisi vizuri ukizinunua. Bila shaka njia ya kufikiria ya wanamazingiria kuwa karibu kila mahali katika uchumi inafaa kuwa kionyo chenyewe. Umazingira ikishakuwa fedhha ya maadili, na kila mtu anainyonya , uwezo wake wa kubadilisha kitu itaenda chini.


Krismasi huu unaweza nunua chochote cha kimazingira kutoka kola za mbwa na simu hadi pia mfuko wa ngozi iliyo dola 850b zisizo na makemikali na imeandikwa “mimi ni dunia.” “Najipenda na najiheshimu,” kwa ufaransa. Kuna hata tovuti la ngono inayopatiana data nyingi kuhusu misitu ya dunia , lakini inapatiana pesa inayopata kutoka uanachama wa kulipa kwa kulinda misistu za mvua. Haijalishi unachofanya siku hizi, inakaa uko sawa bora tu useme ni ya Mama Dunia.”


Alan: Hiyo ni mnara ya kweli sana sana kutoka bwana Rodriguez, kweli sana kwasababu kila kitu ni kauli mbiu. Ni kauli mbiu. Tunasikia maneno za kidini zinazotumiwa kusaidia Mama Dunia. Tunaona tayari wale walio mbele ambao wameimeza yote tayari. Huwa wanatumia wale walio kwa mapindo kupitisha ajenda zao. Watu walio kwa mapindo ndiye mara mingi wale ambao hawako imara na watapigania sababu ambazo ni za kiradikali na hao huwa mara mingi ni vituko wa utawalaji wenyewe. Wanakuwa waongozi wa sehemu za kiradikali katika mwendo za badala. Watu wa Marekani ambao wanaona televisheni pengine kushinda taifa ingine yoyote inapitia mabadiliko kubwa saa hii kwasababu ya hiyo kweli, lakini kuna matumaini ndani ya Marekani kwasababu ya ukubwa wake, kwasababu ya ukubwa wa umma yake na kwasababu ya historia yao. Kuna watu ambao wako na uwezo wa kuona viwango tofauti za kuelewa pengine, lakini wako na kumbuko ya kitu ambayo nchi mingi hazijawai kuwa nayo – na hiyo ni kumbuko ya kitu inayoitwa haki na uhuru. Hiyo ndiyo maana watashambuliwa zaidi kushinda nchi zingine niko na hakika “Silaha za Kimya za Vita za Kimya” zitatumiwa zaidi Marekani kwa tufani na janga kuwafanya wote wafikirie tu juu ya kuishi mbeleni.


Mbinu ya kuunganisha Marekani ni tofauti kwasababu walihitaji 9/11 si kufanya sera zao za kigeni peke, ambayo ilikuwa kwa vitabu tayari, lakini kuwapatia sababu ya kuharakisha mbele na maunganisho, fikra ya Ngome America inatuambia sote, “mipaka ni za kizamani, nchi na mifumo zao za uchumi na ubepari wao, urasimu wao si za ufanisi. Lazima tuziunganishe kwa sababu ya ufanisi, kwa sababu ya usalamiko na tusipofanya hivyo tutaenda chini. Tutawachwa nyuma,” kauli mbiu kubwa. Hiyo ndiyo ilikuwa kauli mbiu ya kuunganisha Ulaya kwa nchi ambazo hazikutaka kujiunga, hivyo ndivyo tangazo za mamilioni na kampeni matangazo zilisema, utawachwa nyuma. Hawakuwai sema utachwa nyuma ya nini. Walisema wachwa nyuma na sasa tunasikia mazungumzo sawa hapa. Kwa nini ubadilishe muundo na kwa nini ubadilishe utaratibu kama inafanya vizuri. Mpangilio. Vile inawekwa pamoja.


Nimeongea mbeleni kuhusu mipangilio. Kwa nini uzibadilishe kama zinafanya ukifuata utaratibu sawa kila saa? Katika Marekani tuko na wengi wa umma ambao wamechukua mafunzo yao vizuri na hawafikiri vizuri nje ya sanduku. Kila kitu unayowaambia kuhusu ukweli ata ukiwaonyesha, haiwafanyi kitu kwasababu wanaishi katika dunia tofauti. Unaona madhara za kutiiwa kasumba kisaikolojia. Hakuna shaka kuna uchaguo kwao kila saa pia, katika akili zao, na inaweza kuwa matokeo tofauti hatimaye, lakini hakuna anayeweza sema ati hawakujua kilichokua kinafanyika.

Nimesoma kutoka wachezi wakuu waliatupatia sehemu huu wa wa hii mfumo – wachezi wazito huko juu wanaotengeneza yanayokuja. Hao ni sehemu wa misingi za kufikiria na taasisi zinazofadhiliwa kabisa, kuleta hii yotr kwa binafsi ya wadogo wanaotawala. Hakukuwa bora zaidi kushinda Bertrand Russell ambao alifanya wengi wa tabaka la wafanyikazi waungane na yeye kwasababu aliongea vile wahindi walikuwa wanasema, “mtu mweupe anaongea na ulimi iliyogawanyika.” Angepatiana hotuba moja ya wafanyikazi waliokuwa nyuma yake na ingine ya wanasiasa wa kiwango yake.


Alisema, “Watu wengi afadhali wakufe badala ya kugikiria. Mara mingi ni hivyo.” Hiyo ndiyo alisema. Hajakosea kukuambia kweli na pia tuko na shida kukubali hizi ata hizi kweli msingi.


Alisema, “Nathani ati mada ambayo itakuwa ya muhimu zaidi kisiasa ni saikolojia ya misa. Muhimu wake imeongezwa na ongezeko ya mbinu za leo za propaganda. Iliyo na ushawishi kushinda zingine ni 'elimu.' Dini iko na sehemu, lakini inayoisha, vyombo vya habari, sinema na radio zinacheza sehemu inayoongezeka.”


Alan: Angeongeza televisheni hapi lakini aliiandika kwa 1953.


“Itatumainiwa ati kwa muda mtu yoyote atakuwa na uwezo wa kushawishi mtu yoyote kuhusu chochote kama anaweza kumpata kama yeye bado ni mdogo na anapatiwa na serikali na pesa na vifaa.”


Alan: Yeye ndiye alishindia chekechea.


“Hii sayansi itasomewa kwa bidii, itafungiwa katika tabaka la watawalaji. Umma haitakubaliwa kujua vile fikira zao zilianza. Mbinu ikishakamilishwa, kila serikali ambayo imekuwa na uwezo wa elimu kwa kizazi moja itakuwa na uwezo wa kudhibiti umma bila kuhitaji majeshi na polisi.Alan: Hiyo imetoka kwa “Athari ya Sayansi kwa Jamii.”(Impact of Science on Society), bado kwake katika ukurasa ya 49 ikienda 50 anasema:


“Jamii za kisayansi bado ziko kwa mwanzo zao. Itatumainiwa ati kwa sayansi ya mwili na saikolojia itapatia maserikali nguvu zaidi juu ya mawazo ya mtu binafsi zaidi ya ile ambayo iko leo ata kwa nchi za kiimla. Fichte aliiweka chini ati lengo ya elimu inafaa kuwa ya kuharibu uhuru ya matakwa, ili, baada ya wanafunzi kutoka shule, hawatakuwa na uwezo, kwa maisha yao yote ya kufikiria ama kufanya kitu kingine isiyolingana na walivyofunzwa.”


Alan: Kitabu sawa.


“Mlo, masindano na amra ya mahakama zitaungana...”


Alan: Kumbuka, nimekuwa nikiendelea juu ya kwasababu ni ukweli. Muhimu sana.


“Mlo, masindano...”


Alan: Hiyo ni chanjo, njia yoyote inayowezekana.


“... na amra ya mahakama zitaungana kutoka miaka za mapema, kutoa tabia na imani ambazo mamlaka wanathani ni mzuri, na na upinzani wowote wa maana haitawezekana kisaikolojia.”

Alan: Mlo, masindano na amra ya mahakama.


“Pole pole, kwa uzazi wa kuchagua, tofauti ya watawalaji na wanaotawala itaongezeka hadi watakuwa aina tofauti. Upinduzi ya watumwa itakuwa haiwezi kama upinduzi iliyopangwa ya makondoo dhidi ya ulaji wa nyama ya kondoo.


Alan: “Athari ya Sayansi kwa Jamii.” Na katika Mtazamo wa kisayansi kwa ukurasa wa 31 anasema:


“Hivyo, watawalaji wa kisayansi watapatia aina ya elimu moja kwa watu wa kawaida, na ingine kwa wale ambao watakuwa wenye nguvu za kisyansi. Watu wa kawaida watatarajiwa kuwa watulivu, wa bidii, sahihi, wapumbavu na maudhui.”


Alan: Tuseme hiyo tena.

“Hivyo, watawalaji wa kisayansi watapatia aina ya elimu moja kwa watu wa kawaida, na ingine kwa wale ambao watakuwa wenye nguvu za kisyansi. Watu wa kawaida watatarajiwa kuwa watulivu, wa bidii, sahihi, wapumbavu na maudhui. Kwa hizi pengine maudhui ndiyo itakuwa ya muhimu kabisa. Ili iletwe utafiti wote wa saikolojia, kitabia na biokemi zitaletwa kwa mchezo. Wavulana wote na wasichana watafundishwa kutoka maika za mapema kulingana, hiyo ni kufanya kile ambacho kila mtu anafanya.”

Alan: Umeona watu walio kando yako wanachofanya? Wote wanafanya wanachofanya.


“Ari itakatishwa tamaa kwa hawa watoto, na kutofuata mamlaka bila adhabu, zitafunzwa kutoka kwa kisayansi. Isipokuwa uaminifu kwa nchi ya dunia...”


Alan: Mwananchi wa dunia. Tunzo za mwananchi wa dunia wanazopatiana; msingi wa Rockefeller.


“na kwa njia yao, wanachama wa watawalaji watahamasishwa kuwa wenye tukio na kujaa na ari.”


Alan: Lazima wabaki na uwezo zao za usalama. Wavulana wakubwa wote wanasema kitu sawa kuhusu hiyo. Hawatajigeuza wenyewe. Hatuaihitaji kwasababu serikali itakuwa inatuamulia kila kitu – hao watendaji wa serikali wote na mabingwa.


“Katika hizo hafla za nadra, wakati ambapo mvujalana ama msichana amepita mwaka ambayo ni kawaida kuamua hadhi ya kijamii anaonyesha ako na uwezo wa akili iliyo sawa na watawalaji, anaweza, baada ya vipimo vinavyofaa, kukuzwa, lakini akionyesha mshikamano yoyote inayosikitisha na washirika wake wa zamani...”


Alan: Kumaanisha tabaka lake, aina yake.


“Waongozi wataamua ati hakuna cha kufanyawa na yeye isipokuwa kumtuma kwa chumba cha kifo kabla uerevu wake iliyo bila adabu imepata wakati wa kuenea upinduzi. Hii itakuwa wajibu wa uchungu kwa watawalaji, lakini sithani wataogopa kuifanya.”


Alan: Amesema ukweli hapo.


“Katika hizo hafla za nadra, wakati ambapo mvujalana ama msichana amepita mwaka ambayo ni kawaida kuamua hadhi ya kijamii anaonyesha ako na uwezo wa akili iliyo sawa na watawalaji...”


Alan: Anaongea juu ya cheo za chini.


“anaonyesha ako na uwezo wa akili iliyo sawa na watawalaji...” kijana huyu atakuwa maudhui na kuwacha washirika wake wa awali...”


Alan: Kumaanisha aingie kwa kikundi yao kabisa na aungane na watawalaji alafu awafanyie kazi.


“anaweza, baada ya vipimo vinavyofaa, kukuzwa, lakini akionyesha mshikamano yoyote inayosikitisha na washirika wake wa zamani...”


Alan: Unajua, wale hapo chini.


“Waongozi wataamua ati hakuna cha kufanyawa na yeye isipokuwa kumtuma kwa chumba cha kifo...”


Alan. Kumua. Watamuua.


“kabla uerevu wake iliyo bila adabu imepata wakati wa kuenea upinduzi.”


Alan: Hiyo imetoka kwa Uangalifu wa Kisayansi. Hakuna kitu ambayo imebadilika katika hii ajenda, na alichokuwa anasema hapo ilikuwa inafanyika tayari alipokuwa anaongea juu ta tunatumaini hii na tunatumaini ile. Ilikuwa inafanyika tayari. Hizi ndiyo wanaandika vitu na bila shaka iko kila mahali duniani leo, karibu iwe kamili.


Mshairi Robert Burns alitoka na mistari mizuri. Kwa shairi moja yake alisema, “Oh mungu angetupatia zawadi ya kujiona, vile wengine wanatuona.” Saa zingine lazima utoke nje yako ndiyo ujione kwa kweli. Kitu ya uchungu hiyo ndiyo maana wengi hawawezi kuifanya. Unapoangalia pahali ambapo fikira zako, tabia, na imani yako inatoka, unapoona ata hizo vitu ambazo unalilia kama nyimbo za taifa na kuendelea, zilipotoka na kwa nini zinafanya kwako vizuri sana alafu kiwanda kubwa cha propaganda imeingiza kwako historia ya uongo inayokuambia kila saa ati vitu zinakuwa bora ili ukatae unachoona mwenyewe.


Majina kitambo zingesema nini leo kama zingeweza kuona America sasa?Mamlaka wanapanga na wamekuwa wakipanga kwa muda mrefu kuchukua kwa njia ya kiimla wakati ambapo watu wa marekani wataamka. Hawataelewa kila kitu lakini watachukiziwa kugundua ati kila kitu walichoamini zimechukuliwa kutoka kwao na hiyo ndiyo maana unaona ujeshi kila mahali kando yako na mfumo wa kiimla mbaya kushinda yoyote iliyofikiriwa na uchunguzi wa kila mtu kila saa. Inaenda kuwa kuzimu na kila hatua ya hii ajenda inahitaji ushirikiano na utii wa kondoo.


Watawalaji huwa wameelewa umma. Umma wanapenda mashuhuri, kile ambacho kila mtu anafanya. Umma wanapenda mashuhuri. Hawaoni atii kile ambacho ni mashuhuri leo inaweza kuwa kinyume ya kile ambacho kilikuwa mashuri 100 ama 50 zilizopita, wakati amabazo wameishia. Wanaikubali tu. Hawakubali. Waneleweka vizuri sana na mapadri wa zamani hadi leo.


Adolf Hitler kwa Mein Kampf ukurasa wa 134 alisema:


“...kwa uongo mkubwa huwa kuna nguvu fulani ya uaminifu kwasababu watu wengi wa nchi huwa wanaweza kupotoshwa kwa urahisi katika tabaka zaidi ya asili yao ya hisia kuliko kwa ufahamu ama kwa hiari; na kwa hivyo kwa unyekevu wa sehemu ya akili yao iliyosahilishawa mno wanakuwa kwa urahisi waathirika wa uongo kuu kuliko uongo ndogo...”


Alan: Walielewa umma kamili. Unajua mtu binafsi ni nini? Mtu binafsi ni mtu asiye mashuhuri. Hiyo ndiyo utu binafsi. Unasema, unafikiria, pengine uko na tabia tofauti na wale kwa umma wanofanya vitu vya mashuhuri; Fikira ya kikundi inafanya vizuri, vizuri sana. Haiwezi kukataliwa. Iko hapo. Unaiona kila mahali kando yako.


Hitler alisema pia:

“Ni bahati gani watawalaji wako nayo ati watu hawafikiri.”


Alisema pia:


“Natumia hisia kwa wengi naweka mantiki kwa wale kidogo.”


Alan: Watu pamoja na dini na hisia wanaweza kudhibitiwa virahisi sana. Hii dini mpya ninavyosema ni tu ile ya mamungu wa kitambo imeyorudiwa tena na tena ambayo wanayoita sasa Enzi Mpya. Ni mwendo wa Enzi Mpya. Dini ni kitu rahisi sana kutengeneza kama uko na pesa na rasilimali na njia za kutumia propaganda ili uiweke uko nje na umma watairukia. Wanapenda vitu ambazo zinawahadi nguvu na hiyo ndiyo sababu ya kweli ya hii dini. Iko hapa pia kutengeneza kauli mbiu, kuleta kauli mbiu ati ati sisi ni moja na wote wataunganishwa kwa kompyuta ya akili na wawe na umoja kwa muda mdogo kabla ya swichi kuu ivutwe alafu hakutakuwa na wao tena. Watakuwa na Nirvana, hali ya kutokuwa. Lengo gani, eh?


Papa Leo X aliyekufa kwa miaka ya 1521 na hii inatoka kwa Encyclopedia Britannica katika matoleo za 9,10,11,12,13 na 14, alisema;


“Imetutumikia vizuri hadithi ya Yesu.”


Katika Encyclopedia ya Kikatoliki kwa ukurasa 133 inasema:


“Kwa kiasi gani familia yetu imefaida kutoka kwa simulizi wa Yesu inaokena kwa Enzi zote.”


Plato alisema, “Ni mtu mwerevu aliyeanzisha mungu.”


Seneca mdogo alisema aliyekufa katika 65 AD alisema, “kila mtu anapendelea imani kushinda matumizi wa hukumu.


Alan: Si huo ni ukweli.


Einstein, “Tabaka la watalawaji wako na kanisa chini la kidole gumba lao. Hii inawawezesha kupanga na kutumia hisia za wengi na iwafanye chombo chao.”


Kwa wana Enzi Mpya wanaothani hii yote ilikuja tu kuwa, mwendo wote na uhindi wanaofuata, na wengi wao hata hawajui ati hiyo yote ni uhindi. Ilirudiwa kuweka Magharibi kwa ufikira – ufikira ambapo wanafundishwa wasiangalie yale mabaya. Kwa maneno mengine, usiangalie zile vitu ambazo pengine utahitaji kujua ili usalimike, angalia tu yale mazuri; na wote wanafundishwa hii na vile ya kupata wanachotaka, ni kweli, hiyo ndiyo ile kitu kingine. Hicho ndicho chambo kuu katika mwendo kuu wa Enzi Mpya: Fikiria na uwe mdosi. Pata unachotaka. Ingiza kitu hii kwako; amini inachosema. Amini inachosema ni na wacha iongoze maisha yako, ama pata mtu wa makadi ambayo atakuambia ile ijayo kwako. Ni rahisi zaidi kusoma majani za chai. Unaweza kunywa hiyo chai na uifurahie pia. Si bei ngumu hivyo.


“Oh binaadamu, kuna chochote ambayo unaweza fanywa usiamini? -Adam Weishaupt, na watu wanafuata hawa watu wa mbele wanaowekwa huko nje ili washangazwe nao kwasababu umma wanataka hizo vitu. Ajabu zaidi unayowapatia na zungmuzo za vitu zisizo za kawaida ndiyo zaidi watafuata mwongozi kwasababu watu wengi wanataka kufanya kama mungu binadamu na wawafuate. Hawajatosheka na mungu aliye nje yao. Wanataka yule ambaye wanaweza kaa na wakule naye.


Bertrand Russell alisema pia, “Watu wanaogopa fikira vile hawaogopi chochote kingine kwa hii dunia, kushinda uharibifu, kushinda kifo. Fikira ni ya kipinduzi, ya uharibu na kutishia, fikira haina huruma kwa

waliopendelewa, misingi na tabia zilizo starehe. Fikira inaangalia katika shimo la kuzimu na haijaogopa. Fikira ni kuu na mwepesi na wa uhuru, taa la dunia, na utukufu kuu wa binadamu.”


Alisema pia, “Watu wengi afadhali wakufe badala ya kufikiria. Bila shaka ni hivyo.”


Pendekezo inaenda mbali, mbali sana. Asilimia sitini ya umma, zoezi badala ya zoezi, wameonyesha wanaweza kushawishiwa mara moja. Asilimia ishrini kufanywa hivyo pia na kazi zaidi kidogo. Kwa hivyo naongea na wale ambao wameshaamka ama wako kwa sindika ya kuamka na wamepitia unyenyekevu ya kugundua ati wamedanganywa maisha yao yote. Hiyo si kitu rahisi kupitia. Tunakwamilia binafsi(Ego) zetu kwasababu lazima tuzilinde katika gharama zote. Lakini, lazima tiwachilie kama tunataka kweli. Si rahisi na watu waliyo na mabinafsi(egos) kubwa kukubali wamekuwa wajinga. Si rahisi lakini hiyo ndiyo lazima ifanywe ili upite hapo.


Yote si mbaya na kweli ambayo ati bado kuna watu uko nje wanaoelewa ambao wamepita ujinga za siasa na uongo za uchaguo na hizo vitu za kawaida ambazo tumepoteza muda zetu nazo kwa muda mrefu, yote si bila matumaini kwasababu sisi ni ushahidi tumeipita. Sisi ni ushahidi inaweza kufanywa na kutoka wengi ninapata mabarua kila saa ati kwa mara ya kwanza wanahisi wanaishi wanapopita hii, kila kitu sasa iko kwa wazi; na hiyo ni miujiza pia, unaopogundua kiasi ya mafunzo iliyoundwa tumeyokuwa nayo kutoka uzazi. Chanjo tulizoptiwa hazikuwa na chochote kufanya na Polio na kuendelea.


Sasa kwangu, nafaa kusema vitu kidogo. Watu hawawezi kuamini ninavyoishi. Haiwezekani kwangu kuelewa ninavyoishi. Napiga sakafu nikikimbia asubuhi. Sina wafanyakazi kunifanyia chochote na lazima nifanye zile vitu za kawaida za kuishi. Ninatengeneza amri ninapozipata. Inachukua milele kuweka utepe kwa zile mabarua kubwa, kimbia kwa kitua cha posta, ambayo si karibu. Niiweke hapo. Niende kwa

kijisanduka changu ambayo haiko karibu kwa nyumba pia. Nichukue posta alafu nirudi nitembeze mbwa. Nitengeneze chakula na kwa muda mdogo niko kwa radio usiku. Alafu baada ya hiyo, kwasababu wameweka mbio ya sputniki yangu kuweka vitu kwa mneti, niligundua kiwanda tata la jeshi ndiye wenye sputniki, wamerudisha mbio yanguu ya mneti kwa nusu iliyokuwa, kwa hivyo nikoo macho hadi saa nne asubuhi. Watu wanajaribu kupiga na naelewa, naelewa hitaji ya kuongea na watu kama wewe, natumaini unajua ati sina saa za kuongea tu na hakuna mtu yoyote chini ya hii jua ambaye atauliza swali moja peke yake. Watanipigia alafu waniulize swali moja kwasababu inaleta zingine mia na masaa zinaita na nilikuwa nakaa kwa simu kutoka asubuhi hadi usiku. Ningechukua simu zote hadi ikawa mbaya sana nilikuwa napoteza uzito. Sikuwa nafanya chochote. Sikuwa hata na muda wa kula, kwa hivyo nakuwa imara kwangu kwasababu ya usalama; na hakuna pumziko, siku saba kwa wiki na huwa kuna watu lazima nirudie. Kuna watu uko nje ambao nimeambia nitawapigia na inarudi nyuma wiki kiasi. Niko na orodha yao na bado sijawafikia. Kuna kazi mingi hivyo hapa.


Hata hivyo, ndiyo hawa sisi katika winta. Tumepitia miaka ingine. Saa ya kuzaliwa upya inavyoitwa wakati ambapo kwa siku tatu jua itaanza kusafiri zaidi ikipanda na hatimaye itaanza kuenda magharibi inapozaliwa tena na masiku kwa pole pole zitaanza kuwa refu na kung'aa zaidi. Saa hizi, chini ya hii theluji kulikuwa na uvuguvugu na bado sijafungua mlango ya sehemu ya nyumba iliyo chini ya ardhi. Sitaki kuvaa koti la kuokoa langu ili niende chini huko, lakini lazima nifanye hivyo, bila shaka. Tulikuwa tunapata uvuguvugu wa januari. Inafanyika wiki moja , njia moja ama inigine, lakini hii inaendana na wakati. Kitu moja ambayo bado ni kawaida. Ingawa wanafukiza mbinguni kusini chini Florida na inavuma huku na hiyo ndiyo pengine imetupatia yeyuka wa theluji. Chini ya theluji unajua unaweza kuapa ati unasikia mbu zikishangilia baada ya Krismasi, hizi bilioni za mbu zikishangilia kwasababu zinajua wakati wa jua zitatoka nje zinikule. Sina shaka kila moja zao ziko na jina yangu kwao. Zinanipenda na ninachoka, kusema kweli kuchangia damu kwa asili. Nakua kama mwenye anemia na ni wabaya sana nathani wanakuwa wabaya zaidi. Nathani wanakuwa wabaya zaidi kwasababu wanazalishwa alafu wanatolewa na hiyo si mzaha kwasababu imekubaliwa kabla wamefanya hizi vitu na mbu na tunaishi kwa nyakati ambazo masayansi zinatumiwa kwa kimya kila saa.


Katika kati kati ya winta, ambapo mwangaza bila kitu, mara mingi tunafikiria juu ya mwaka uliopita. Hiyo ndiyo maana yake, wakati wa akisi na upya, ambapo unaangalia nyuma kwa huo mwaka uliopita alafu unapangia ijayo. Mabadilikokuu zinakuja. Sote tunafaa kujitayarisha kiakili na “kiroho,” hiyo neno inayotumia vibaya leo, kiroho, kwa yale yanayokuja. Ninavyosema, kuna tumaini. Kuna tumaini kama wata kama mimi wanaweza kufika juu. Sijakubaliwa kuwa “hapo juu”. Niliuliziwa kwa stesheni za redio kwasababu watu wengi wamekuwa wakifuata mazungmuzo zangu na wakauliza mamaneja wa hizi stesheni, wakawashambulia hadi sikuweza kupuuzwa zaidi; kwa hivyo unatumia njia ambazo uko nazo saa zile bado ziko.


Nani anajua tutakuwa na uwezo wa kusema tunachofikiria? Saha watu kama mimi wanaozungmza kuhusu vitu ninayozungmzia. Alafu nimekuwa na jaribio mingi za kunitoa kwa vipindi na watu wanaojulikana vizuri sana. Watu wanaoniambia nichukuwe pande yao, alafu vitu zitakuwa mzuri nikikubali ajenda yao na niliposema “hapana sitadanganya umma,” moja wao aliniambia

“nitapigia vipindi zote na nikutoe.” Hawa ndiye wanasimamia nguvu za giza kwasababu lazima wachanganyishe watu kwa muda hizi na wachukue wale wanaoamka ili wawazungushe kwa mauongo, ambapo itaisha kwa pahali sawa ambapo wote wataweka kompyuta kwa akili yao na wawe moja. Hiyo ndiyo kauli mbiu wanaohubiri hatimaye, ufahamu uliogeuzwa. Ikuzoeshe. Ikufanye uitake. Ikuahadi ujinga nyingi. Ikupatie ajabu nyingi na umma wanataka kuiamini pia, alafu utakuwa na kompyuta yako kwa akili na nyote mtakuwa moja kwa “nirvana” ambapo haitabidii ufikirie ama uwe na uwezo wa kufikiria – hasa kile watawalaji wanataka.


Ubinafsi nii kitu mpya. Nimepitia hii kabla. Hadi 1800 tulikuwa mfumo gumu, ujuaji mdogo sana kuhusu dunia kubwa katika nchi mingi. Hiyo iliwekwa kwa watawalaji wadogo. Watumwa wakulima walifanya kila kitu kijamii. Ubinafsi haikupatiwa nafasi na baadaye ilipopata nafasi watu kidogo waliichukua. Hawapedi – wanaogopa kuwa tofauti; na lakini kuwa tofauti na kuwacha akili yako itange kwa maeneo yasiokubaliwa inakuwa furaha akili yako ikifanya inavyofaa kufanya. Kwa hivyo tutapitia siku za giza na tutarudi kwa mwanga tena springi ikija, na Hamishi mbwa anafanya vizuri. Afya yake iko mzuri na ni rafiki mzuri na anaweza kuwekana na mim, na hiyo inasema kitu. Bado tunaenda kwa matembezi. Si za muda ya kutosha saa hii kwasababu sina muda wa kutosha, lakini natumaini hiyo itabadilika siku moja na si rahisi kufika mbali na hiyo theluji yote.


Hatimaye natumaini kupata usaidizi kuchukua mzigo wa hizi barua pepe zote na hizo vitu zote zingine ambazo mtu mwingine anaweza kunifanyia, kutuma mabarua na kuendelea. Hivyo naweza kukaa na niandike vitabu zaidi. Sitafanya mavideo tena kwasababu zinachapishwa alafu zinauzwa pahali pengine na kuna wale wameokuwa wakiishi kutoka kwa kila kitu nimekuwa nikizungmzia na wanazipatiana bure. Ninauliza watu watumie akili yao. Angalia kila kitu. Fikiria kwa mwenyewe. Uliza matazamo zako pia na vitu unazoamini na hitimisho na fikiria unazozifikia, na usiogope kama maoni zako ni za wachache. Hiyo ni ishara mzuri.


Kutoka Hamish na mimi, kwa hii Krismasi ya utulivu hapa Ontario, Canada ni usiku mzuri na mungu ama miungu ama Hallelujah, inayomaanisha jua imeinuka, chochote ambacho inayokufanya uhisi vizuri na uwasiliano na kitu iende nawe.


Kabla niende, ama nimalize huu mzungmuzo, nilitoa moja wa gitaa zangu za kitambo. Kitu ambayo bado sijachezea kwa miaka kumi nilipowachulia kila kitu na zaidi kidogo za miaka kumi nilidungwa mashindano za kuenda nje ya nchi na nikagonjeka vibaya baada ya wiki mbili. Nilijua ilitoka kwa hizo mashindano na vidole zangu zilifura kama zile za mtu mzee baada ya miaka za kugonjeka na nilijua muundo. Nilijua inavyoenda lakini niliona mtaalamu bado na alipitia muundo, niliyojua na akasema “oh, zitafura alafu baada ya hiyo neva sitakufa na uchungu itaenda alafu mkono zako zitarudi kwa kawaida.” Nilisema hapana na kwa hivyo nikazifunga na utepe kwa nguvu ili nirudishe mfuro chini na nikafanya hivi kwa miezi tatu, katika winta nilitumia msumeno kwasababu sikuwa na kuni na niligeuza vidole zangu kila wiki kidogo hadi zikarudi chini. Tangu hapo nimefanya kazi mingi gumu na ya uzito kwa hivyo nisamehe kama niko kutu kidogo kwenye hii gitaa.


Mbeleni niliifikiria na nikasema unajua sina chochote mingi cha kupatia watu na ningependa ata kuwashukuru wale ambao wamenisaidia na nishukuru wafasiri kazi yote ambayo wamefanya. Inachukua muda, kazi mingi, kwa hivyo hi ndiye zawadi yangu ya krismasi kwao na kwa wasikizaji na usicheke ninapofanya hizo kosa zote kwasababu imekuwa miaka tangu nishike gitaa.